Waziri Nchemba awatahadharisha wauza dawa za kulevya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba
akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu
ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute
shughuli halali za kujiingizia kipato.
Waziri
Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi
na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Aidha
Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia
na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.
Naye
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha
anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya
mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.
Pia
Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto
zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika
miaka ya hivi karibuni.
Mawaziri
walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais
kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu
Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na
Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara
baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo
na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment