AVEVA AUNDA BARAZA LA WAZEE SIMBA.
Kwa muda mrefu Simba haikuwa na Baraza la Wazee wa klabu huku watani wao wa jadi, Yanga wakilitumia la kwao kufanya mambo mbalimbali zikiwamo fitna za kiungozi."RAIS wa Simba, Evans Aveva, ameonekana kuiga mbinu za Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji baada ya jana kutangaza kuunda Baraza la Wazee wa klabu hiyo ya Msimbazi.Katika hafla ya kuzindua kadi za watoto wanaotaka kuwa wanachama wa Simba jijini hapa leo, Aveva amesema kuwa klabu hiyo iliyoanzishwa 1936, imeunda Baraza la Wazee litakalokuwa linatoa ushauri kwa uongozi juu ya mambo mbalimbali ya klabu.Baraza hilo linaongozwa na Mwenyekiti Omary Mtika na wajumbe ni Ally Hassan, Abdulsharif Zahoro, Chuma Suleiman 'Bi. Chuma' na Omary Moshi.MJENGWA.
Post a Comment