Kauli ya Serikali Kuhusu Gazeti la Tanzanite Lililomwandika Mange Kimambi
Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema imewaita wahusika wa gazeti la Tanzanite ambalo limesambaa mitandaoni likiwa limebeba katika ukurasa wa mbele habari inayomhusu Mange Kimambi.
Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dkt Abbas amesema kuwa, amelazimika kuwaita wahusika hao ambao atakutana nao leo ili aweze kusikiliza upande wao baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma ya gazeti hilo.
Nakala ya gazeti hilo linaloonekana mitandao linaonyesha kuwa lilipaswa kutoka Machi 5, kwani hata usajili wake ni wa mara moja kwa wiki (kila jumatatu).
Post a Comment