Nape: Viongozi Afrika kunga’ang’ania madaraka ni ushetani
Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amesema ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani.
Kupitia ukurasa wake wa twitter leo Machi 5, 2018, Nape ameandika kuwa ni lazima ushetani huo upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla haujaota mizizi na kusambaa.
Nape ambaye amewahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Rais John Magufuli na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Harrison Mwakyembe amekiri kuwa twitter ni yake ingawa hakuwa tayari kufafanua zaidi.
“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa!” unasema ujumbe huo wa twitter.
Post a Comment