Header Ads

WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI NA LORI LA TAKA DODOMA

Watu sita wamefariki papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria kugongana na lori mjini Dodoma.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gillece Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Machi 4, 2018 majira ya mchana wakati daladala iliyokuwa na abiria zilipogongana na lori hilo.

"Taarifa zaidi nitazitoa baada ya kufuatilia lakini kwa ufupi ajali hiyo ipo na watu sita wamekufa na wengine sita wapo katika hospitali ya rufaa ya mkoa na hali zao sio nzuri," amesema Muroto

Na Habel Chidawali - Mwananchi

No comments