Header Ads

WANASIASA WAASWA KUACHA IMANI ZA KISHIRIKINA

 


Wanasiasa nchini wametakiwa kuachana na imani za kishirikina hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kwani kufanya hivyo kunachochea hasira ya Mungu kwa Taifa.

Hayo yamesemwa na Askofu wa makanisa ya Harvest Ministries of Tanzania (HMT) alipokuwa akihubiri leo ibaadani katika tawi la kanisa hilo lililopo Mkolani Geita kwa Mchungaji Paul William, "Mimi nipo kwenye maombi naombea uchaguzi huu,kila mwanasiasa anayeenda kwa waganga kutafuta uchawi ili ashinde namwomba Mungu asishinde na badala yake wale wanaomtegemea Mungu ndio washinde,mambo kama haya yanasababisha mauaji kwa watu wasio na hatia ikiwemo watoto kutekwa na kutolewa figo na viungo vingine na mambo mengi tunayoyasikia,mambo haya yanachochea hasira ya Mungu na kuleta laana katika nchi" Amesema Askofu huyo.

Askofu Mpogomi pia amewataka waumini wa kanisa hilo kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii kwa kutenda matendo mema yenye kumpendeza Mungu na watu pia. Ameongeza kuwa wakristo ni barua inayopaswa kusomwa na kila mmoja hivyo wasiwe na mambo ambayo yatauchafua mwili wa Kristo.

Kanisa la Harvest ni miongoni mwa makanisa yaliyopo nchini Tanzania huku makao yake makuu yakiwa Magogo mjini Geita na mpaka sasa kanisa hilo linayo matawi manane mkoani Geita,Mwanza na Tabora na lengo ni kueneza matawi kila kona ya Tanzania.

No comments