Header Ads

Polisi waongea kuhusu Maandamano yanayozungumzwa Mitandaoni

Leo February 26, 2018 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amezungumza na Waandishi wa habari kuhusu Maandamano ambayo yanaandaliwa Mtandaoni na  kupangwa kufanyika nchini.
Kamanda Mambosasa amesema “Kuna kuhamasishana kupitia mitandao kuna watu wanaendelea kuhamasisha Wananchi kuvunja sheria, wanataka wajiandae kwa maandamano, wanafanya hivyo wao wakiwa wamekaa mahali ambapo ni salama”.
“Wanataka kuwaingiza Watanzania wengine kwenye shida, ninawaomba Watanzania amabao siku zote wanajua thamani ya amani wajiepushe na uchochezi huo, ninachotaka kusema kwa Kanda Maalum ya DSM yeyote ambaye atashindwa kupokea haya ninayosema asijutie yatakayotokea” -Mambosasa
CREDIT:Millard Ayo

No comments