Diamond Akabidhiwa Rasmi Leseni ya Wasafi TV na Wasafi Redio
Hatimaye Bosi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platinumz amepata leseni ya kuziweka hewani redio na televisheni za Wasafi zilizobatizwa jina la ‘Wasafi Radio na Wasafi TV’.
Diamond amevuka maji na kuzipata leseni zake visiwani Zanzibar ambapo alikabidhiwa na Wizara ya Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.
Mkali huyo wa ‘Sikomi’ jana aliwashirikisha mashabiki wake habari hiyo njema iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, siku chache baada ya kuonesha picha akiwa anajaribu mitambo ya mradi huo mpya.
Kupitia Instagram, ameandika ujumbe akiambatanisha na picha za leseni hizo, akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
==>Diamond ameandika:
(Leo tulikabidhiwa Rasmi Leseni ya @wasafitv na @wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni , Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma…..Shukran Nyingi ziifikie Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamuhuri nzima ya Muungano wa Tanzania… Ma raisi wetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison Mwakiyembe….
Tamanio letu ni kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji ambao pengine hawajapata nafasi bado….kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi tusingekuwepo….lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni…. ) #HiiNiYetuSote.
Ni dhahiri kuwa Wasafi TV na Redio zitagusa anga la Tanzania Bara na Visiwani.
Post a Comment