Header Ads

Picha: Davido amuanika mwanamke anayedhaniwa ni mpenzi

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameachia picha akiwa na mwanamke anayedhaniwa ni mpenzi wake mpya aitwaye Chioma katika mitandao.

Davido ambaye kwa sasa anafurahia mafanikio ya kimuziki kutokana na  kuingiza pesa nyingi katika tamasha lake la 30 Billion amemuanika mwanamke huyo walipokuwa nchini Uingereza.

Picha ya wawili hao ilipigwa wakiwa katika chumba huku wakionyesha kuwa katika dimbwi zito la mahaba, na imewekwa na hitmaker huyo wa ‘If’ katika mtandao wake wa Snapchat. Hata hivyo Davido hajasema jambo lolote kuhusu picha hiyo.

No comments