Dancer wa kike anayetumbuiza jukwaani bila ‘kuvaa kufuli’ azuiwa kuingia Zambia (Picha)
Mnenguaji/Dancer aliyejizolea umaarufu nchini Afrika Kusini, Zodwa Wabantu azuiwa kuingia nchini Zambia wikiendi iliyopita ambapo alikuwa na tamasha nchini humo.
Serikali kupitia Waziri wa Wizara ya Mambo ya Utamaduni na Dini nchini Zambia, Godfridah Sumaili imesema kuwa sababu za kumzuia Zodwa ni kulinda maadili ya taifa lao kwani kumruhusu ni kuruhusu wasichana nchini humo kupotoka kimaadili.
“Hataweza kuingia nchini kwa njia yoyote ile, inajulikana wazi kabisa nchi hii ni ya wakristo na inatambua umuhimu wa dini na thamani yake kwenye jamii, kama taifa hatuwezi kuruhusu vitu kama hivi vifanyike. Yaani mwanamke acheze jukwaani bila chupi haiwezekani,“amenukuliwa Waziri Bi. Godfridah kwenyegazeti la serikali la The Times of Zambia.
Zodwa ambaye anasifika kucheza jukwaani bila kuvaa nguo ya ndani amejipatia jina kubwa sio tu nchini Afrika Kusini bali ukanda wote wa nchi za kusini mwa bara la Afrika.
Zodwa alitarajiwa kutumbuiza Jijini Lusaka Jumapili ya wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya uzinduzi wa album ya Pandemonium ya msanii wa muziki nchini humo, Karasa Karayo.
Mwezi Januari mwaka huu msanii kutoka Nigeria, Davido alitangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa atamtumia mrembo huyo kwenye video zake zijazo za muziki.
Tazama baadhi ya picha za Zodwa akiwa anaonesha uwezo wake jukwaani na muonekano wake.
Post a Comment