Header Ads

WAZIRI PROF MAKAME MBARAWA AMEITAKA TCRA KUKOMESHA WIZI WA MITANDAO.

Waziri wa mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa ameitaka bodi mpya ya mamlaka ya mawssiliano Tanzania TCRA kuhakikisha inasimamia kikamilifu ukomeshaji wa wizi wa mitandao ikiwa ni pamoja na uondoaji wa urasimu wa kiutendaji katika utoaji wa leseni za mawasiliano.
Waziri huyo mwenye dhamana katika sekta za mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi mpya ya mawasiliano nchini nakuitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano kati yake na menejiment ya TCRA na maafisa wa wakawaida.
Prof Mbarawa pia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kuendelea kutoa adhabu kali kwa makampuni ya mawasiliano yanayokiuka sheria za mawasiliano nakuonyesha kukerwa na ubovu wa baadhi ya mitandao ya simu ambayo imekuwa kero kwa watumiaji kutokana na ubovu wa mitambo yake.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo amemhakikishia Prof Mbarawa kuwa bodi hiyo imejipanga kutekeleza maagizo yote matatu ya waziri yakiwemo ya kudhibiti uchochezi kwenye mitandao, wizi wa mitandao ikiwa ni pamoja na kusimamia ubora wa mawasiliano.

No comments