Header Ads

Trump akosoa China kwenye Twitter

 Donald Trump- Rais Mteule wa Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametuma ujumbe kwenye Twitter yake ukikosoa China dhidi ya sarafu yake na operesheni katika bahari ya 'South China Sea'.

'' China ilitushauri wakati ikipunguza dhamani ya sarafu yake na kujenga kambi ya kijeshi South China Sea? Sidhani walifanya hivyo '', ulisema ujumbe wa Trump kwenye Twitter.

Wiki iliyopita Trump alizua mzozo wa kidiplomasia na China baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu na Rais wa Taiwan. Hatua iliyopelekea China kuilalamikia Marekani. Marekani imekosoa China kwa kupunguza dhamani ya sarafu ya Yuan ikisema hatua hiyo ilipendelea mauzo ya China nje ya nchi.

Pia imeitaka China kuachana na umiliki wa visiwa vinavyozozaniwa na mataifa jirani katika bahari ya 'South China Sea'. Marekani imetuma manowari zake katika eneo hilo, na pande zote zimelaumiana kwa kulifanya eneo hilo kuwa chini ya nguvu za jeshi. China imesema hatua yake inanuia kutumika kwa maslahi ya raia.

Kwa sasa Marekani imewekea kodi baadhi ya bidhaa kutoka China ikiwemo magurudumu na vyuma.
Donald Trump amesema ataweka kodi ya asili mia 45 ya bidhaa zote kutoka China.

Donald Trump na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen waliwasiliana kwa njiya ya simu

Mazungumzo ya simu kati ya Donald Trump na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen ni ya kwanza kwa kiongozi wa Marekani kufanya na utawala wa Taiwan tangu mwaka wa 1979 ambapo uhusiano kati ya pande mbili ulisitishwa.

Taiwan imedai kuwa taifa huru, lakini Mamlaka za Beijing eneo hili ni moja ya majimbo yake. China hata imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo Taiwan itajitangazia uhuru.

No comments