Header Ads

Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki  Dunia jana jioni  baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui FC ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.

Ismail Khalfan  alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Serikali ya mjini Bukoba.

Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.

Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC  na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.


No comments