Header Ads

Polepole Ateuliwa Kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Kuchukua Nafasi ya Nape Nnauye

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi kuchukua  nafasi ya  Nape Nnauye

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia ukurasa wake wa Twitter zinaeleza kuwa kikao chaHalmashauri Kuu ya Taifa kimemteua Polepole kushika wadhifa huo.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kimefanyika leo ambapo miongoni mwa mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimemteua Ndg @hpolepole kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi.


No comments