|
Wanafunzi wakiwa katika mahafari ya kidato cha nne wakifatilia kwa makini kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika sherehe hizo. |
|
Wanafunzi ambao ni wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kakubilo wakiingia katika ukumbi wa sherehe. |
|
Skauti akitoa heshima kwa Mgeni Rasimi Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi wakati alipokuwa akiwasili katika viwanja vya shule hiyo. |
|
Mgeni Rasimi Akimvikwa sikafu ambapo ni moja kati ya heshima kubwa kwa jeshi la Skauti. |
|
Mgeni Rasimi akikagua paredi ya wanafunzi huku akiongozwa na kamanda wa skauti shuleni hapo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi na Kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya Mji wa Geita,Beatrice Balige wakikata utepe kwaajili ya uzinduzi wa sherehe za kuwaaga wahitimu. |
|
Kikosi cha Skauti kikionesha ukakamavu wake mbele ya mgeni rasmi shuleni hapo. |
|
Mwenyekiti wa shule Peter Sumuni akijitambulisha na kuainisha changamoto zilizopo shuleni hapo ni pamoja na uhaba wa kukosekana walimu wa masomo ya sayansi. |
|
Mkuu wa shule ya Sekondari Kakubilo,Said Swelehe akitambulisha meza kuu wageni waliokuwepo na walioambatana na mgeni rasmi. |
|
Zoezi la ugawaji wa vyeti likiendelea. |
|
Wanafunzi wa kidato cha nne wakiimba shairi katika mahafari yao ya kidato cha nne. |
|
Diwani wa kata ya kakubilo akitoa nasaha kwa wahitimu wa kidato cha nne. |
|
Kaimu afisa elimu wa Sekondari halmashauri ya mji wa Geita Beatrice Belige akielezea mikakati ya kuongeza walimu wa somo la sayansi ambalo ni changamoto ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi shuleni hapo kukimbia kombi hiyo. |
|
Mgeni rasimi ambae ni Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi akijaribu kusisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kujituma zaidi katika kufikia malengo yao. |
|
Wananchi wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasimi katika mahafari hayo. |
|
Mkuu wa wilaya akiwaaga wananchi na kusalimiana nao wakati alipokuwa akiondoka katika viwanja vya sherehe hiyo. |
PICHA NA MAELEZO:MADUKA ONLINE
Wanafunzi wilayani Geita wametakiwa kusoma kwa bidii na kuachana na tabia za kuharakia maisha pindi wanapokuwa katika masomo.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya hiyo,Mh Herman Kapufi wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafari ya kwanza ya kidato cha nne shule ya sekondari kakubilo.
Amesema kuwa ni vyema kwa wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu kwa kujituma kwa bidii na maarifa ili kuendana na dunia ya sayansi na teknolojia.
“ Nyie mabinti na nyie vijana hata kama umemaliza mtihani wako wa kidato cha nne ni marufuku kuoa wala kuolewa mpaka matokeo yatoke yani ikitokea umeoa au kuolewa na matokeo yametoka umefaulu tutakuja kukuchomoa huko huko na utakwenda shule na Yule aliyekudanganya tunampeleka jela anakwenda kuzeekea huko huko hatutakuwa na huruma na swala hili dhidi ya wale ambao wamekuwa wakisitisha masomo ya wanafunzi”alisisitiza Kapufi.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Rauliani Sweke amefafanua kuwa ni vyema kwa kila mzazi kujenga desturi ya kuwahimiza watoto wao kupenda elimu.
“Tunatambua kuwa elimu ni ufunguo wa maisha hivyo nawaomba wazazi wenzangu wahimizeni watoto wenu wapende shule kwani Dunia kwa sasa imebadilika.”alisema Sweke.
Sanjari na hayo shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu wa somo la sayansi hali ambayo imempelekea kaimu afisa elimu sekondari halmashauri ya mji wa Geita Bi Beatrice Balige kuelezea jitihada ambazo zipo kwa sasa katika kutatua changamoto ya kukosekana kwa walimu wa masomo ya Sayansi.
Kwa upande wao wahitimu shuleni hapo Devid Samuel na Yasinta Joshua ,wamewaomba wanafunzi wanaobaki shuleni hapo kusoma kwa bidii na maalifa huku wakimtanguliza Mungu mbele.
Post a Comment