PICHA 9: Reli ndefu zaidi duniani iliyojengwa chini ya ardhi kwa miaka 17 kuzinduliwa Uswisi
Uswisi imeingia kwenye headline ambapo Reli ndefu zaidi ambayo inapita chini ya ardhi imepangwa kufunguliwa wiki za hivi karibuni baada ya miaka 17 ya ujenzi, reli hiyo kwa mara ya kwanza ilianza na mchoro mwaka 1947 lakini ujenzi wake ulianza miaka 17 iliyopita.
Majaribio ya treni kwenye reli hiyo yanatarajiwa kuanza wiki ijayo June na abiria wa kwanza kabisa kwenye treni hiyo wanatarajiwa kuanza December, Miamba tani milioni 28.2 imetumika kujengea reli hiyo.
Imeelezwa kwamba kuanzishwa kwa reli hiyo kutasaidia suala zima la usafiri ambapo Muda wa kusafiri kati ya Zurich na Millan utapungua kutoka masaa mawili na dakika 40 na itakuwa saa moja ambayo ni haraka zaidi ukilinganisha na ilivyo hivi sasa.
Post a Comment