NESI AKAMATWA KWA WIZI WA GLOVES KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA GEITA
Fatuma Salumu ambaye ni mhudumu katika Hospitali ya Rufaa mkoani Geita anatuhumiwa kwa wizi wa gloves piece 77.
Mwanadada huyo ambaye ni nesi katika kitengo cha CTC katika Hospitali hiyo ambacho kinashughulikia masuala ya UKIMWI alikamatwa leo Alfajiri majira ya saa kumi na mbili akijaribu kutoroka nje ya geti na ndipo vijana wa kikosi cha Geita Security Guard walifanikiwa kumkamata.
Mbali na hayo Mkurugenzi wa Geita Security Guard alielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea huku akiongeza kuwa hiyo ni mara ya pili kwa mtuhumiwa huyo kukamatwa na anashangaa kumuona bado anaendelea na kazi.
Aidha ametaka mamlaka husika iingilie kati ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo vya wizi pamoja na ufisadi kwani mamlaka yake inafanya kazi yake ipasavyo kwa kuwakamata watu wanaokiuka maadili ya kazi na kuwafikisha sehemu husika
Post a Comment