Header Ads

Tazama Gari la kifahari la Yahya Jammeh lenye thamani ya TZS milioni 800.....Inadaiwa Kakomba Fedha zote kabla ya Kuondoka.


Yahya Jammeh aliyeitawala Gambia kwa miaka 22, hatimaye jana aliondoka nchini humo na kwenda kuishi uhamishoni baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Disemba Mosi mwaka jana.

Jammeh alishindwa na kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vya upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchni Senegal alipoapishwa kuwa Rais wa Gambia baada ya Jammeh kukataa kutoka madarakani awali.

Yahya Jammeh alipokuwa akiiongoza Gambia aliweza kujinunulia vitu vingi vya kifahari na moja wapo ni gari lake la kifahari aina ya Rolls Royce.

Gari hili ambalo kwenye viti vyake ameandika jina lake, lina thamani ya kati ya fedha za kitanzania milioni 500 hadi milioni 800. Rolls Royce ni moja ya magari ya kifahari na ya kipekee duniani ambayo mara nyingi hutumiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha.

Gari hili la Yahya Jammeh liliwashangaza rais wengi wa Gambia lilipokuwa likikatisha katika viunga vya mji wa Banjul kumpeleka kiongozi huyo uwanja wa ndege tayari kuondoka nchini humo.

Licha ya kuwa Jammeh aliondoka nchini Gambia jana huku wananchi wakishangilia kwa furaha, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alikomba fedha katika hazina ya nchini hiyo na kuiacha katika ukata mkubwa wa fedha.

Taarifa kutoka katika kambi ya Rais Adama Barrow zinaeleza kuwa dola za kimarekani milioni 11 zilichukuliwa katika hazina ya nchi hiyo.

Yahya Jammeh tayari amewasili nchini Equatorial Guinea ambapo ndipo ataishi.

Hapa chini ni picha zaidi za gari hilo la kifahari;

Hapa ni sehemu ya magari ya Yahya Jammeh yaliyopo uwanja wa ndege wa Banjul Gambia, baada ya ndege toka Guinea kuzuiliwa kuyachukua.




No comments