Header Ads

WALIMU WASHUSHIWA KIPIGO NA WAZAZI KISA ADHABU KWA WANAFUNZI.

Mwalimu Medard Zacharia aliyevamiwa na kupigwa na wazazi baada ya kutoa adhabu kwa mwanafunzi ambaye alizimia shuleni Hapo

Mwalimu Deogras Ristone akielezea masikitiko yake kutokana na kupigwa na wazazi kwenye shule ambayo wanafundishia

Baraza la shule likijadili na kuweka maadhimio ya kutokufundisha hadi pale wananchi ambao wametenda kitendo cha kuwapiga walimu watakapochukuliwa hatua za kisheria.

Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Geita,Mwalimu John Kifimbi  akielezea kusikitishwa kwake juu ya kitendo ambacho kimefanywa na wananchi.


Walimu wawili wa shule ya Msingi Isabilo kata ya Bugurula wilaya na Mkoa wa Geita wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa fimbo na wananchi waliovamia shule hiyo kulipiza kisasi baada ya walimu hao kudaiwa kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi mmoja aliyepandisha mapepo.

Tukio la kushambuliwa kwa walimu hao limetokea Januari 25,mwaka huu na kwamba walimu 10 wa shule hiyo wamegoma kuingia madarasani kufundisha wakiomba serikali iwahamishe kutoka shuleni hapo kwa kuwa wamefedheheshwa na wananchi.
Walimu walioshambuliwa ni Medard Zacharia na  Deograsi Ristone ambao wanamajeraha sehemu mbalimbali za miili yao. 

Mwalimu Mkuu Msaidizi Athuman Augustine anasema Chanzo cha tukio hilo ni walimu kutoa adhabu ya viboko vitatu vitatu kwa kila mwanafunzi ambaye hakwenda kufanya zamu ya usafi wakati wa likizo na ndipo wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo mmoja wa wanafunzi waliopewa adhabu alipandisha mashetani.

“Wakati wa kutoa adhabu mtoto mmoja anayedhaniwa kuwa na mapepo,alianguka na kuzimia hali iliyoamsha gadhabu kwa wazazi na kusababisha wananchi kuivamia shule na kuanza kuwashambulia walimu kwa fimbo”Alisema Athuman.                                                                                                                                                                                                                                                             
Mwl,Medard  Zakaria,ameeleza kuwa yeye alitoa adhabu hiyo kama mwalimu ambaye alikuwa zamu siku hiyo .

“Nilitoa adhabu kama mwalimu ambaye nilikuwa zamu lakini nashangaa cha kusikitisha wakati nawaachia wanafunzi mmoja wao ambaye jina limehifadhiwa alianguka akiwa darasani na kuanza kupiga kelele kutokana na hali hiyo sisi kama walimu tulikwenda kumtazama lakini hali yake haikuwa njema ilitulazimu kupiga simu Hospital ya Nzera kuomba msaada wa kuja kuchukuliwa wakati tulipokuwa tunaendelea na jitihada hizo ndipo kundi la wazazi  likafika likiwa na hasira wakiuliza kwanini umewapiga watoto wetu sikujibu kitu kutokana na hilo mmoja kati ya wazazi alinivamia na kuanza kunichapa fimbo mbele ya wanafunzi huku akiniuliza ni kwanini unawapiga wanafunzi ndio hali ilivyokuwa”alisema Zakaria

Mwalimu Deogras Ristone,ameiomba serikali kupitia  kwa afisa elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kuwahamisha sehemu hiyo kwani kwasasa hawana amani ya kuendelea kufundisha wala kufanya kazi kwenye mazingira ambayo wamefanyiwa kitendo cha kudhalilishwa  mbele ya wanafunzi ambao wanawafundisha .



No comments