BEI YA UMEME YAMWONDOA MKURUGENZI MKUU TANESCO.

Mhandisi Felschemi Mramba

Taarifa kutoka Ikulu
Rais John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felschemi Mramba kuanzia jana, Januari 1, 2017.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo. Kabla ya uteuzi huo, Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Post a Comment