Serikali yatoa kauli uhaba wa chanjo ya pepopunda
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha taarifa za kuwapo kwa uhaba wa chanjo za kinga dhidi ya ugonjwa pepopunda, na kusema kuwa ina chanjo za kutosha.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo Bw. Nsachris Mwamwaja amesema habari iliyotolewa leo na gazeti moja la kila siku, ilikuwa imepitwa na wakati na ya kupotosha kutokana na waliohojiwa kwa sasa hawapo madarakani.
Amewataja waliohojiwa kuwa ni Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Stanley Dinagi ambaye yupo nje ya nchi kimasomo, na Mganga Mkuu wa Serikali Donald Mmbando ambaye hayupo katika wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu sasa.
Amesema Ilala kuna dozi 35,000 zilizosambazwa Tarehe 06.12.2016 na mahitaji yao kwa mwezi dozi 7110, Temeke kuna dozi 33,000 zilisambazwa tarehe 06.12.2016 mahitaji yao kwa mwezi ni dozi 7620 na Kinondoni dozi 11,000 zilisambazwa tarehe 07.12.2016 mahitaji yao kwa mwezi ni dozi 9210.
Kwa hivi sasa hakuna upungufu wowote wa chanjo ya pepopunda nchini kwani kuja jumla ya dozi 599,000 katika bohari ya kuu taifa na wanatarajia kupokea shehena nyingine ya dozi 1,200,000 wakati wowote ili kuhakikisha kwamba hakuna uhaba wa chanjo.

Post a Comment