Header Ads

WAKAZI KATIKA SOKO LA NYANKUMBU MKOANI GEITA WAKO KATIKA HATARI YA KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA UCHAFU ULIOKITHIRI.

Nyankumbu ni moja kati ya masoko maarufu mkoani Geita hasa kwa wakulima,lakini ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa uchafu,ikiwa ni pamoja na watu kujisaidia nyuma ya majengo ya soko hilo kutokana na huduma ya choo kutokuwepo pamoja na kuwa choo kilishajengwa lakini Halmashauri ya mji idara ya afya haijakabidhiwa na mamlaka husika.Akizungumza ofisini kwake juu ya uchafu huo Afisa afya wa mkoa Bw. Masese alisema wanasubiri kukabidhiwa choo hicho kilichojengwa na wafadhili chini ya mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Mwanza,na kuwataka wananchi hao kuendelea kutumia choo cha zamani ambacho hata hivyo kimeshajaa,Nae Philimon Charles Matonge katibu wa soko hilo amesema Halmashauri haijachukua hatua zozote pamoja na kukaa nao.
 Hii ni sehemu ya nyuma kwenye moja kati ya majengo ya soko la Nyankumbu ambapo watu hujisaidia haja zao zote ambapo mvua zinaponyesha maji hutiririka kuelekea ndani ya soko hilo.
 Moja ya sehemu ambapo mama ntilie hupika na kuhudumia wateja hata hivyo sehemu hiyo pia imetazamana na majengo ambayo watu hujisaidia nyuma yake.

 Choo cha soko cha zamani ambacho kimejaa na hata hivyo watu wanaendelea kukitumia.
Jengo jipya la huduma ya choo katika soko la Nyankumbu ambalo inadaiwa halijakabidhiwa rasmi kwa matumizi. 


 Ndani ya soko wananchi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
Huu ni uchafu ambao umeenea kila mahali katika soko hilo. habari na Paul B William.

No comments