Header Ads

KUWA MAKINI KATIKA KUCHAGUA RAFIKI; Pastor Paul William

 Na Pastor Paul William




Nakusalimu kwa jina la Yesu popote pale ulipo unaposoma ujumbe huu.
Leo napenda kukushirikisha neno hili fupi ambalo Roho Mtakatifu amenipa baada ya kusoma kitabu cha mwanzo.
Kuna watu wengi wamejikuta wakiingia kwenye matatizo makubwa,madeni,kesi na hata kupoteza kila kitu kwa sababu ya aina ya marafiki waliokuwa nao ama watu wao wa karibu.
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 3:1 Biblia inasema " Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke,Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu,Msile matunda ya miti yote ya bustani?"
Hapa napata picha kuwa Eva na nyoka walikuwa ni marafiki wa karibu mno,walitembeleana kila mara na kuzungumza,unaweza kuniuliza mchungaji unajuaje? Kumbuka kabla ya dhambi kuingia hapakuwa na uadui wowote kati ya viumbe vingine na mwanadamu na pia haingewezekana nyoka kukurupuka tu na kuanza kuongea na mtu ama kiumbe asichokuwa na mazoea nacho inaonekana wazi ni marafiki waliokuwa wameshibana kiasi cha kuelezana masuala ya siri.
Eva alimwona nyoka kama rafiki wa karibu anayezungumza naye kipindi mumewe akiwa hayupo,lakini jambo ambalo mama Eva hakuelewa "Adui wa mtu ni yule wa nyumbani mwake mwenyewe" na pia shetani hawezi kutumia mtu wa mbali usiyemjua kuangamiza maisha yako.
Mpendwa msomaji,jaribu kuwa makini sana na watu wengine unaowaita "watu wa karibu" wapo kina nyoka" wasiopenda mafanikio yako licha ya kuwa mkiwa wote watakuchekea na zaidi ya yote shetani atawatumia kukuharibu,ndio hao watapeleka picha yako kwa mganga,kuzoa mchanga wa miguu yako,kupeleka jina na nguo yako ili kufunga hatima yako.
Utajuaje rafiki huyu hafai? Ni rahisi, 
Ukiona mtu wako wa karibu anakushauri uende kwa mganga,kunywa pombe,kuvuta bangi,kuwa na michepuko mkwepe haraka sana maana huyo ni shetani amekuja kwa sura ya rafiki yako.
Zaidi ya yote uwe makini katika kuchagua watu wa kuambatana nao,sio kila mtu anaweza kufaa katika kutimiza kusudi lililoko ndani yako. 
Mungu wa mbinguni akubariki. Kwa mawasiliano zaidi nipigie +255742133926 pia namba hii inapatikana whatsapp





No comments