Header Ads

MILIONI 173.5 ZATOLEWA KWENYE VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU GEITA

Mkuu wa mkoa mhandisi Robert Gabriel akikabidhi hundi ya fedha kwa Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu cha Ludete Bw,Julius Mashindano.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wanakikundi wakati wa zoezi la kuwakabidhi mikopo ambayo wamepatiwa na halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wajasiliamali kutokuogopa kukopa fedha.

Baadhi ya wanavikundi vya ujasiriamali wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.


Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa kiasi cha Sh,Milioni 173.5 ikiwa ni mwendelezo wa halmashauri kuhakikisha asilimia 10% ya makusanyo ya ndani inatolewa kwa vikundi vya wanawake ,vijana na walemavu ili kuweza kuvisaidia kujinyanyua kiuchumi kupitia shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya za ujasiriamali.

Katika azima ya kuwawezesha wananchi,hususani wanawake,vijana na walemavu halmashauri hiyo imeendelea pia kutoa elimu na kufanya uhamasishaji katika kata 37 kwa lengo la kuhimiza wananchi kujiunga kwenye vikundi vya ushirika na kuchangiana mitaji yao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiongezea kipato.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw,Ali Kidwaka ametaja changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo ni pamoja na wakopaji kutokuwa na utayari wa kurejesha feza hizo kwa wakati na wanakikundi kuhama kutoa eneo moja kwenda jingine bila ya kutoa taarifa.

Aidha kwa upande waka Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amewasisitiza wajasilia mali hao kutokuwa na uwoga wa kukopa na pia kuzitumia fedha hizo kwenye matumizi sahihi ya kujikwamua kimaisha.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elisha Lupuga amewasisitiza wanavikundi ambao wamepatiwa mkopo huo kutokutumia kinyume na makubaliano ambayo yamepangwa na serikali bali wafanyie shughuli ambazo zitawasaidia kuinua vipato vyao.

Mkuu wa Mkoa Huo,Mhandisi Robert Gabriel ameziomba taasisi za kifedha kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa fedha.

Baadhi ya wanavikundi ambao wamepatiwa fedha hizo wameishukuru serikali kwa namna ambavyo imeendelea kujitoa kuwasaidia wananchi ambao wanamaisha ya chini.

No comments