Header Ads

Mchezo wa Mtibwa Sugar Vs Buseresere kupigwa nyamagana

Mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya Buseresere hatua ya 16 bora kombe la Azam Sports Federation Cup sasa umehamishiwa katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza badala ya uwanja wa Kahama kama ilivyotarajiwa hapo awali na kutarajiwa kupigwa siku ya Jumapili ya tarehe 25.02.2018.
Mtibwa inayomilikiwa na kiwanda cha kutengeneza sukari bora nchini Mtibwa Sugar imefikia hatua hii ya 16 bora kwa kuwafunga Villa Squad ya Dar es laam 2-1 katika hatua ya 64 na pia kuwafunga Maji Maji rangers katika hatua ya 32 ya Azam Sports Federation Cup.
Vodacom Premier League:
Jumatatu hii ya tarehe 19 .02.2018 wana tam tam wanataraji kujitupa uwanjani kuwakabili Ruvu Shooting kutoka Pwani katika mchezo wa ligi kuu bara utakaofanyika katika dimba la Manungu Complex.

No comments