Hashim Rungwe aungana na CHADEMA Kumuombea Kura Salumu Mwalimu
Mheshimiwa Hashim Rungwe Spunda Mwenyekiti (CHAUMMA) jana Februari 15, 2018 aliungana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumnadi mgombe Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu.
Akiwa kwenye mkutano huo ambao ulifanyika katika Kata Ya makumbusho Viwanja Vya Vegas Rungwe alisema kuwa wana Kinondoni hawapaswi kumchagua mgombea wa CCM kwa kuwa ni msaliti na amekuwa muongo.
"Serikali hii ya CCM inajidai sanaa inafanya propaganda kwenye Radio na kila mahali lakini mimi naomba niulize wangapi wamekuja hapa hawana kitu mfukoni, mna hela nyie?
"Wananchi hali zao mbaya watu hawana kitu. Jamani tunampima kiongozi kwa mambo anayofanya tumeona tawala nyingi lakini mmeshawahi kuona utawala wa namna hii?
"Yaani polisi ndiyo wanafanya serikali ifanye kazi yaani bila ya polisi hawafanyi kazi, polisi ndiyo wamewekwa mbele yaani ukisema hivi unakamatwa"
Rungwe aliendelea kuelezea juu ya sakata lake la kukamatwa na polisi siku za karibuni
"Mnakumbuka mimi nilikamatwa juzi juzi hapa yaani hakuna kitu chochote cha maana mpaka sasa mimi ni Wakili na Wakili kazi yake ni kusaini nyaraka, nimesaini nyaraka za watu na hao watu wenye pesa walikuwa wakitoa maagizo mlipe huyu na huyu na mimi nalipa sasa mimi nimefanya kosa gani?
" Hawa watu ni wabaya na haya ni mambo ya serikali ya CCM, hakikisheni kwamba serikali ya CCM mnaiondoa msikubali Mtulia awe Mbunge wenu. CCM ndiye wanaiharibu nchi hii" alisisitiza Rungwe
Post a Comment