TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YALAANI VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO.
Tume
ya haki za binadamu na utawala bora imelaani juu ya vitendo vya kikatili
vilivyoibuka tena hivi karibuni katika baadhi ya mikoa vya kufukua makaburi ya
watu wenye ualbino kunakotokana na imani za kishirikina na kuitaka serikali
kuongeza juhudi zaidi katika kupambana na watu wanaofanya uhalifu huo.
Mwenyekiti
wa tume hiyo Bw.Bahame Tom Nyanduga amesema hayo jijini Dar es Salaam mara
baada ya kikao kilichohusisha wadau mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali
kukemea vitendo hivyo vya kikatili na kusema kuwa bado juhudi zaidi
zinahitajika katika mapambano hayo ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.
Bw.Nyanduga
pia amezitaja changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma juhudi mbalimbali za
serikali na vyombo vyake katika kupambana na vitendo hivyo ikiwemo mkanganyiko
wa takwimu juu watu wenye ualbino waliopotea ambavyo vinakwamisha
ushughulikiaji wa wahalifu huku ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu (DPP) ikitaja
kesi ambazo zimeshashughulikiwa mpaka sasa.
Post a Comment