Header Ads

WEZI WA MIFUGO WAIBA NA KUACHA NAMBA ZA SIMU KASAMWA.

Ng'ombe wakinywa maji katika bwawa la Kasamwa,bwawa ambalo binadamu na mifugo hulitumia kwa pamoja.
Wananchi wa kata ya Kasamwa wilaya na mkoa wa Geita wameiomba serikali kuchukua hatua za kisheria kuhusiana na swala la wizi wa mifugo linaloendelea kwa kasi mkoani hapa.

Hayo wameyasema mbele ya  mbunge wa viti maalum  Geita upendo peneza kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati walipokuwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa ng’ombe,mkutano huo ulikuwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi.
 
Mbunge wa viti maalumu mkoani Geita(CHADEMA) Mh.Upendo Peneza akiwa na aliyekuwa diwani wa Kasamwa Fabian Mahenge.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya mh.Upendo Peneza,  mwenyekiti wa mtaa wa NMC Kasamwa  kwa niaba ya wananchi Bwana Boazi  Mathayo  amesema kuwa  suala la wizi wa mifugo limekua ni kero kubwa kwani baadhi ya wezi wa mifugo hiyo wamekuwa wakiacha namba za simu pindi wanapoiba ili watumiwe fedha ndipo mifugo hiyo iweze kupatikana.
Mathayo  ameongeza kuwa  wananchi wa mtaa huo wanakabiliwa na changamoto ya maji hivyo wameiomba serikali  kusaidia kutatua kero hiyo  ilikuwezesha wananchi wa kata hiyo kupata maji salama

Aidha mheshimiwa Peneza  amelaani vikali vitendo hivyo vya kikatili vinavyozidi kukithiri mkoani hapa na kuwaomba wananchi kushirikiana kwa  pamoja na kutoa taarifa katika vitengo husika ili kukomesha uhalifu huo pamoja na unyanyasaji wa wananchi unaoendelea mkoni Geita.

No comments