WACHIMBAJI WADOGO 400 WALIONDOLEWA KATIKA MACHIMBO YA MWASABUKA MKOANI GEITA,WAREJESHWA
Zaidi ya wachimbaji
wadogo 400 wa dhahabu,waliokuwa wameondolewa katika machimbo ya Mwasabuka
yaliyopo wilaya ya Nyang’whale mkoani Geita kwa madai kwamba eneo
hilo ni mali ya mgodi wa dhahabu wa Acacia,baada ya mashimo yao kufukiwa kwa
amri ya mkuu wa wilaya hiyo, hatimaye hii leo wamerejeshwa tena katika maeneo
yao.
Uamuzi wa kuwarejesha
wachimbaji hao katika eneo hilo lililokuwa chini ya ulinzi mkali wa askari
polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi umetangazwa na mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi mkoani Geita Mh.Joseph Kasheku msukuma.
Mkuu wa mkoa wa Geita
Meja Jenerali Mstaafu Elias Kyunga ambaye amezuru katika eneo hilo la machimbo
ya Mwasabuka,ameliagiza jeshi la polisi kutoendelea kuwabughudhi wachimbaji
hao.
Mapema alfajiri, askari
wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU ) kutoka mkoani Geita kilikuwa kikiwafukuza baadhi ya wachimbaji
waliokuwa wameanza kurejea katika mashimo yao,jambo ambalo wamedai linakiuka
agizo la Rais Dk.John Magufuli.
Post a Comment