Sheikh Khalifa Khamis alivyolalamika Waislam kuminywa na Serikali Kuu, TRA na Vyombo vya Dola.
Sheikh maarufu nchini Khalifa Khamis amewahi kuishtumu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuwa ina lengo la kuikwamisha dini ya Kiislam. Aliishtumu TRA kuwa na masharti ya kibaguzi dhidi ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, alisema masharti hayo yamejaa hila, udhalilishaji. Alidai nia ya TRA ni kukwamisha shughuli za BAKWATA hapa nchini kwa kisingizio cha kodi za magari lakini nia yao kukwamisha dini ya Kiislamu.
Alizitaka taasisi za Kiislamu nchini kukataa maagizo kutoka TRA.
Pia aliishtumu Serikali ya awamu ya 5 kuwa inawanyima waumini wa dini ya kiislamu nyadhifa katika teuzi mbalimbali na alisema kuwa baadhi ya Waislamu wamekuwa wakiondolewa nafasi zao serikalini sababu ya dini yao.
Aliongeza kwa kuitaka Serikali ibadilishe sheria ya ugaidi nchini kwa sababu ni kandamizi na Waislamu wengi wamekuwa wakikamatwa kwa kisingizio cha kuwa magaidi na hawapelekwi mahakamani na mpaka sasa kuna baadhi wako jela bila kufikishwa mahakamani, alitoa mfano wa masheikh wa Zanzibar wanaoshikiliwa kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani.
Angalia video hapa chini;
Post a Comment