Pande mbili zinazovutana ndani ya CUF zafikishana mahakamani.
Upande
mmoja wa uongozi wa chama cha wananchi CUF unaopinga maamuzi ya ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kumtambua Prof Ibrahimu Lipumba kama
mwenyekiti wa chama hicho, umeamua kufungua shauri mahakama kuu
kuitaka mahakama kutoa zuio la msajili wa vyama kuacha kufanya kazi za kisiasa.
Shauri
hilo limefunguliwa katika wakati ambao vigogo wawili wa ngazi ya juu wa chama
cha CUF Prof Lipumba na Maalim Seif wakionekana dhahili kukigawa chama hicho,
ambapo upande unaomuunga mkono Maalim Seif unasema umeamua kufungua kesi kwa
lengo la kuiomba mahakama kuu kutoa zuio kwa msajili wa vyama vya siasa
kuachana na shughuli hiyo kwa madai amekuwa chachu ya mvutano ndani ya chama
hicho.
Wakati
kila upande wa vigogo hao wawili wakionekana kuwa na uchu wa kushinda katika
mvutano huo wa uongozi, jumuiya ya vijana wa CUF mkoa wa Dar es Salaam wao
wanaamini chini ya uenyekiti wa Prof Ibrahimu Lipumba chama chao kitakuwa
salama zaidi.
Licha
ya viongozi wa juu wa chama hicho kugawanyika vipande, taasisi nyingine ambazo
zimekumbwa na mgawanyiko huo ni pamoja na jumuiya ya vijana, bodi ya udhamini
ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na wanachama wenyewe wa CUF.
Post a Comment