Mkoa wa shinyanga watajwa kuwa kinara kwa ndoa na mimba za utotoni.
Mkoa
wa shinyanga unatajwa kuwa kinara kwa ndoa na mimba za utotoni ambapo asilimia
59 ya watoto wa kike huolewa chini ya umri wa miaka 18 wengi wao ikiwa kutoka
familia maskini na maeneo ya vijijini.
Wakati
dunia ikijiandaa kuadhiisha siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa
kila oktoba11,wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto inasema
katika tafiti ambayo imefanywa na ofisi ya taifa ya takwimu imeonyesha mkoa wa
shinyanga unaongoza kwa kuwa na tatizo hilo ikifuatiwa na mikoa ya Tabora na
Mara ambapo serikali inasema haitosita kuwachukulia hatua wazazi ambao
huwaozesha watoto wao chini ya umri wa miaka 18.
Wadau
mbalimbali waliojikita katika kulinda haki za mtoto wa kike wanasema ni vyema
elimu ikaendelea kutolewa kwa watoto wa kike tangu ngazi ya elimu ya awali ili
watambue haki zao mapema kutokana na athari za ndoa za utotoni ikiwemo athari
za kihisia na kisaikolojia.
Maadhimisho
ya siku ya mtoto wa kike duniani kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani
Shinyanga yakishirikisha wizara na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi
huku kauli mbiu ikiwa mimba na ndoa za utotoni zinaepukika,chukua Hatua
kumlinda mtoto wa kike
Post a Comment