Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kubuni mbinu ya kumlinda Tembo.
Wakati tembo wakiwa wamepungua nchini kutoka tembo 110,000 hadi tembo 15,000 serikali imesema inatafuta mbinu sahihi ikishirikisha wadau katika kutafuta mbinu sahihi ya kumlinda tembo ili kuongeza idadi ya tembo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya tunduru Bw.Juma Homera wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya kitaifa ya kupinga mauaji ya tembo yaliyofanyika wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ambapo amefafanua kwa kusema kuwa serikali inatafuta njia za kumlinda tembo katika maeneo yanayoathiriwa na tembo nchini ili tembo na wananchi wabaki salama.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kikosi cha kupambana na ujangili kanda ya Kusini Bw.Joshua Mmari amesema serikali inatambua majanga yaliyowakumba wananchi mwaka huu kwa kusababishwa ;na tembo ambapo wananchi na mali zao vimeangamia hivyo inakamilisha taratibu za kulipa vifuta machozi na vifuta jasho na kwamba yako mashamba hewa yaliyoingizwa katika mchakato huo na kuchelewesha ulipaji.
Naye Meneja wa Shirika la utunzaji wa mazingira duniani(WWF) hapa nchini Bw.Simon Lugandu amesema kuwa kampeni kubwa ya kitaifa na kimataifa ya kumuhifadhi Tembo inafanyika kwa kuwa Tembo wamepungua nchini kutoka kutoka Tembo 110,000 hadi kufikia Tembo 15,000.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya kupinga mauaji ya Tembo mwaka huu ni dunia tuungane kumlinda Tembo.
Post a Comment