WANANCHI KYERWA WAHIMIZWA KULIMA MAZAO YANAYOKOMAA KWA MUDA MFUPI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akitembelea eneo la kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa kujionea ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulivyoathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera na kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista akiwa ziarani wilaya ya Kyerwa na kujionea mazo la viazi ambalo pia linaweza kulimwa wilayani humo.
(Picha maelezo na Eleuteri Mangi, Kyerwa, Kagera).
………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi, Kyerwa, Kagera
Ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera umemlazimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.
Athari hiyo ya ukame imemlazimu Waziri Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla w0aanze kulima mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze kuwapunguzia adha ya upungufu wa chakula unaotokana na kutegemea zao la ndizi pekee.
Akiwa katika kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama aliongea na wananchi wa kata hiyo ambapo alisema “Mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa, msiendelee kutegemea zao moja tu la chakula la ndizi, ni lazima mkubali sasa tuende kwenye mazao mengine ya chakula, limeni mihogo, limeni mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa muda mfupi, vinginevyo tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi kwa hali ya hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.
Waziri Mhagama aliyataja mazao hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi kuanzia miezi mitatu ndiyo yanaweza kuwa mkombozi wa katika kukabiliana na upungufu wa chakula na kuwahakikishia wananchi chakula cha kutosha hatua ambayo itawafanya waendelee na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao.
Mkulima wa kata hiyo Shakiru Issa anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima mazao mengine zaidi ya ndizi na kahawa ambayo yanamuongezea kipato ambapo yeye analima pia zao la viazi mviringo kwa ajili ya chakula pamoja na kuuza hatua inayomsaidia kumuongezea kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.
Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Waziri Mhagama amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya kuchoma mapori moto mara moja kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha maisha ya watu, kupoteza mazao shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo ndiyo kivutio kikuu cha mvua.
Aidha, ziara hiyo wa Waziri Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya Itera ambapo amemwagiza Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aende kufanya tahmini ya hali ukame ilivyo athiri wilaya hiyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri Mhagama ametoa wito na kumuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu pamoja kulima zao la ndizi, aanza haraka kampeni ya kuwahamasisha wananchi hao kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ambayo yataweza kuwapatia chakula cha kutosha kwa mahitaji yao ya kila siku.
Post a Comment