Header Ads

GEITA:WANANCHI WA KATA YA KASAMWA NA KANYARA WALALAMIKIA KUTOKAMILIKA KWA UJENZI WA BWAWA LA MAJI.

Mbunge wa viti maalum Jimbo la Geita Upendo Peneza akitoa ufafanuzi juu ya kuhakikisha anafikisha kilio cha wananchi kwenye halmashauri ya mji wa Geita na kama itashindikana swala la Bwawa atalifikisha Bungeni.
Mh,Peneza akiteta jambo na Fabiani Mahenge katika eneo la Bwawa la Kasamwa.

Muonekano wa Bwawa linalolalamikiwa na wananchi wa Kata hizo Tatu.

Ng'ombe wakinywa maji katika Bwawa ambalo wananchi wamekuwa wakitumia maji hayo kwa mahitaji ya kila siku ya familia ikiwemo kunywa na kupikia.

Ukaguzi wa maeneo hayo ukafanyika hapa wananchi wakimwonesha eneo hilo ambalo limeshamalizika kutengenezwa namna lilivyo kwa sasa.

Wananchi wakielezea namna ambavyo wamekuwa wakikereka na kile ambacho kimefanyika baada ya agizo la Rais la kujenga Bwawa hilo.


Mama akiwa amebeba ndoo akitokea kuchota maji ya Bwawa hilo.


Wananchi wakiimba wimbo wa kutaka haki ya kupatiwa maji.




GEITA:Wananchi wa kata ya Kasamwa,Kanyara na Bung’wangoko Wilayani na Mkoani Geita ,wamelalamika Kutokamilika kwa Bwawa la Kasamwa na kwamba  kuhusiana na pesa zilizotolewa hazijulikani zilitumika  kwa namna gani kwani hali bado ni tete kutokana na sehemu hiyo kutumika kunyweshea mifugo.

 Katika hali  isiyo ya kawaida wala ya kuridhisha BAHEBE STAR imefika katika kata hiyo na kukuta baadhi ya mifugo , ikiwemo Ng’ombe wakinywa maji huku  akinamama wakichota  maji hayo kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

Thabiza Selemani ni mkazi wa kata ya kasamwa,ameeleza kuwa maji hayo kwa sasa ni machafu kwani tangu Bwawa hilo kutengenezwa kutokana na agizo la Rais dk John Pombe Magufuli hali ni mbaya limechafuka kwa kiasi kikubwa.

“Kwa namna maji haya yalivyo kwa sasa ni bora ambayo yalikuwepo kwani yamevurugika zaidi kwa sasa hatuwezi kufulia wala kupikia mara nyingi wanatumia watu kujengea nyumba kiukweli tunaomba serikali isikie kilio chetu maana tunaangamia.”Alisema Thabiza.

Almas Ngongoseke, yeye amesema kuwa Bwawa halijajengwa bali limesafishwa kidogo tu ni kisha watu kuwakabidhi wananchi.

Mbunge wa viti maalum jimbo la Geita(CHADEMA) mh Upendo Peneza amefika katika bwawa hilo na kuwahaidi wananchi kufikisha kilio chao ngazi za juu kutokana hujuma iliyofanywa ya ujenzi wa Bwawa hilo.

“Lakini ukiliangalia hili Bwawa halifanani na kufanyiwa kazi kwa milioni 79 wananchi walitegemea kwamba Bwawa hili lingekuwa refu kwenda chini na tope yote ingweza kuondolewa ili wananchi wapate maji safi na salama vile vile Mh,Rais alitoa agizo la kutenga sehemu ya kunywea mifugo na sehemu ya kuchotea maji ninawaahidi wananchi swala hili nitalifikisha halmshauri ya mji na hata Bungeni”Alisema Upendo.


Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita ,Mwandisi Modesti  Apolinary,Amefafanua juu ya madai hayo kuwa tatizo ni wananchi kuendelea kupeleka mifugo katika  Bwawa hilo kutoa ufafanuzi juu ya swala.

Imeandaliwa na Joel Maduka.

No comments