Joseph Mgile akiwa ameweka pozi la kupigwa picha na waandishi na baada ya kamera kumzonga zonga.
Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) Mkoani Geita imemfikisha mahamani mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu GGM Joseph Mgile kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono wakati wa kutoa ajira ndani ya mgodi huo.
Wakisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Geita Ushindi Swaro wanasheria wa takukuru Kelvin Murusuri akishirikiana na Felister Chamba wameiambia mahakama hiyo kuwa tarehe moja juni 2015 Joseph Mgile akiwa afisa mwajiri wa mgodi wa GGM aliomba rushwa ya ngono kutoka kwa Saida Honga kwa ili kumpatia kazi.
Wanasheria hao wameendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa pamoja na Saida kuwa na vigezo vyote vya kupata kazi lakini alishindwa kupata kazi kwa kigezo cha kukataa kutoa rushwa ya ngono.
Mara baada ya kumaliza kusoma shitaka hilo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kuomba kupatiwa dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kusaini hati ya milioni saba kila mmoja.
Mshitakiwa huyo amekosa vigezo vya dhamana na kupelekwa rumande na kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa kesho.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
|
Post a Comment