MKUU WA WILAYA YA GEITA AAGIZA KUHAMISHWA KWA MTENDAJI WA KIJIJI CHA BUJURA
Mkuu wa wilaya ya
Geita Herman Kapufi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita
kuhakikisha anamuhamisha Mtendaji wa Kijiji cha Bujura Sekile Mhagwa kuanzia jana kutokana
na kuwa na tuhuma za kutumia fedha kiasi cha Sh.Millioni 9
kinyume na matumizi ya fedha hizo,
Miongoni mwa fedha
hizo kulikuwa na fedha za watoto waishio katika mazingira
magumu na zingine za watu ambao wameathirika na Virusi vya Ukimwi (VVU) na
pesa nyingine ya mfuko wa Jimbo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa
Wilaya kufanya Ziara yake ya Kikazi yenye lengo la kuzungumza na
Wananchi na kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba
Wananchi wa Wilaya ya Geita katika mkutano na Wananchi Kata ya Bujura
Diwani wa Kata hiyo Amina Kanijo amefikisha malalamiko yake mbele ya
Mkuu wa Wilaya akimtuhumu mtendaji wa Kata kutumia Fedha kinyume na
utaratibu uliokuwa umewekwa.
Na kutokana na malalamiko hayo
ilimlazimu Mkuu wa wilaya ya Geita kutoa maagizo ya kuhakikisha mwalimu
ambae ametuhumiwa na matumizi ya fedha kukamatwa lakini pia na
mtendaji hata kama amelipa fedha hafai kuendelea kubaki katika kituo
hicho cha kazi hivyo amemuagiza Mkurugenzi kumpatia uhamisho wa
kwenda kufanyia kazi mahali pengine.
Pia Herman Kapufi aliwaagiza
Watumishi wote kuhakikisha wanakuwa na maadili katika kuwatumikia
Wananchi na kuachana na tabia ya kuwa kero katika jamii
wanazoziongoza.
Post a Comment