Header Ads

SUALA LA WAFUNGWA KUNYONGWA, SERIKALI YATOA KAULI.


       Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Harrison Mwakyembe (Kulia) akizungumza katika kikao baina yake na watendaji wa                                  wizara yake Mkoani Mwanza. 
                         Kutoka Kushoto waliokaa ni Kaimu Katibu                         Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijira, Mkuu wa                               Wilaya ya Nyamagana (Kaimu Mkuu wa Mkoa wa                                                 Mwanza) Baraka Konisaga.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imesema bado haijafikia uamuzi wa kutekeleza hukumu ya kunyonga wafungwa, wanaohukumiwa kunyongwa hadi kufa kutokana na makosa ya jinai ikiwemo mauaji.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe, alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza, wakati akizungumza na Watendaji wa idara mbalimbali za Serikali ikiwemo Magereza pamoja na Mahakama, kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza.

Dkt.Mwakyembe alisema kuwa suala la kunyonga wafungwa linahitaji maridhiano kwa kuwa utekelezaji wake unaweza kuliingiza taifa katika migogoro isiyo ya lazima ikizingatiwa kwamba watetezi wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati mbalimbali wamekuwa wakilipinga.

Katika hatua nyingine Dkt.Mwakyembe alikemea vitendo vya ukatili na mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambalo limeshamiri katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa huku Mkoa wa Mwanza ukiwa kinara ambapo amesema Serikali haiwezi kukubali vitendo hivyo kuendelea kujitokeza.

No comments