Rais Magufuli Kuzuru Rwanda Kwa Mara ya Kwanza Tangu awe Rais.....Atazindua Daraja la Rusumo na Kufanya Mazungumzo na Rais Kagame Mjini Kigali
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.
Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na Rais Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzania na Rwanda na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania Rais Magufuli atasafiri kwa gari.
Post a Comment