Header Ads

MSANII DAYNA NYANGE ADAI ANAPENDA KUVAA NGUO ZA KUACHA KIUNO

Dayna
Msanii wa kike, Dayna Nyange amedai anapenda kuvaa nguo ambazo zinaacha wazi sehemu ya kiuno chake.
Akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Dayna amewataka watu kuacha tabia ya kuingilia maisha ya watu wengine.
“Unajua usipende kumjaji mtu kwa mavazi, mimi si mvaaji wa vikaptula au vinguo vifupi napenda tu kuvaa nguo inayoniacha ‘kakiuno’ tu kidogo wazi, kwa sababu napenda” alisema Dayna.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Angejua’.

CHANZO na Bongo5

No comments