VINCENT KIGOSI (RAY) WA BONGO MOVIE AKANUSHA MADAI YA KUJICHUBUA.
Msanii wa filamu nchini Tanzania Vincent Kigosi(Ray)amekanusha madai kuwa anajichubua.
Mwenyewe asema kila mtu akiwa na maisha mazuri anaweza kubadilika.
"Kwanza sijichubui,tatizo unajua baadhi ya watanzania walio wengi hawaelewi,mimi sijichubui ila maisha yamebadilika,unajua unapokuwa na maisha magumu ya kwanza,unashindwa kujikimu,kujinunulia nguo,yaani kufanya unachokitaka kwa muda unaoutaka,unakuwa mweusi kwa sababu huna hela ya kujikimu!
Unapokuwa na maisha mazuri,kwako kuna AC,kwenye gari lako kuna AC,hupati jua huwezi kuwa mweusi",alisisitiza.
Pia ukishakuwa Star lazima muonekano wako uwe tofauti kidogo.Hawa wanaoona mimi najichubua,labda wanaona vibaya!Mimi sijichubui na waache waendelee kuzungumza kwa sababu mtanzania huwezi kumzuia kuzungumza"Alisema Ray.
Post a Comment