Mkongo mpya wa mawasiliano chini ya bahari kuja Afrika Mashariki
Kampuni ya Liquid Telecom ipo katika hatua za mwisho kufanikisha mradi mpya wa kutandaza mkongo wa mawasiliano wa baharini ambao pamoja na kuunganisha kusini mwa Afrika pia utaunganisha na Mashariki ya kati pamoja na Ulaya.
Iwapo mkongo huu utakamilika basi itakuwa ni habari nzuri kwa watumiaji na watoa huduma wa intaneti hapa Tanzania kwani itakuwa ni nafasi ya kuongeza ufanisi na ubora wa huduma katika sekta hii.
Bosi wa kampuni hiyo ya Liquid Telecom ambayo imejikita zaidi nchi za kusini mwa Afrika alikuwa na mazungumzo na aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki DR Richard Sezibera alipotembelea makao makuu ya jumuiya.
Nkusi amesema kwamba Cable hii itapita katika njia ambayo haina watumiaji wengi zaidi kwenda Ulaya, hii itasaidia watoa huduma na watumiaji wa tanzania kuweza kapata intaneti yenye spidi kubwa na pia ya uhakika zaidi.
Mkongo huu utatambazwa chini ya bahari ukiambaa na ukanda wa Afrika Mashariki kuelekea katika bahari ya Shamu ambapo baada ya kuvuka bahari hiyo mkonga huu utaishia Ulaya, utakapoweza kuunganishwa na mikonge mingine.
Aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki aliahidi ushirikiano na wawekeaji hao huku akitilia mkazo umuhimu wa jumuiya ya afrika mashariki kuunganishwa na ulimwengu.
Kwa mtanzania wa kawaida kuongezeka kwa mkono wa cable ya chini ya bahari ni dalili nzuri kwamba watoa huduma kama vile mitandao ya simu itakuwa na nafasi kubwa ya kufanya machaguo juu ya mkongo upi utumike kitu ambacho kinaweza kuchangia kushuka wa gharama au kuongezeka kwa ubora wa huduma za intaneti.

Post a Comment