Header Ads

MBOWE APINGANA NA WABUNGE WENZAKE WA UKAWA JUU YA MAPENDEKEZO YA BAJETI IJAYO YA SERIKALI..!!!


BAADHI ya wabunge wamepongeza mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/17, yaliyowasilishwa na Serikali kutokana na bajeti hiyo kwa mara ya kwanza, kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa fedha za nje, lakini pia kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha katika matumizi ya maendeleo.
Akizungumza baada ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka huo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema mambo mema yamefanywa.
Alisema mambo matatu makubwa yakitekelezwa, itakuwa imetibu kiu ya watanzania ya muda mrefu, moja ni kupeleka fedha nyingi kwa maendeleo na kubana matumizi ya kawaida na pili imepunguza utegemezi wa wafadhili, kufadhili bajeti ya nchi. Alisema hilo ni jambo jema na kusisitiza kuwa msingi iwekwe ya kuimarisha.
“Ukomo wa bajeti ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, hili nalo katika serikali ya awamu ya tano wameliona na kweli tuwaunge mkono, sio kila kitu tuone kibaya, cha msingi tuwape nafasi tuone watamalizaje huko mbele kwenye utekelezaji”, aliongeza Mbowe.
Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alisema mapendekezo ya bajeti hiyo, hayana uhalisia na huenda yasitekelezeke, kwa kuwa yameegemea zaidi katika mafanikio ya muda mfupi yaliyopatikana katika ukusanyaji wa kodi na faini za wakwepa kodi.


Kuhusu ushauri wake wa namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mapendekezo ya bajeti hiyo, mbunge huyo alisema “waulizeni CCM, hiyo si kazi yangu”.
Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) alisema baada ya kumaliza habari ya faini za kodi na wale waliokwepa kulipa kodi, makusanyo yatashuka kwa kiasi kikubwa. Alishauri kuibuliwa kwa maeneo mengi, yaliyotekelezwa yanayoweza kulipishwa kodi, ikiwemo eneo la bahari ambalo kwa mujibu wake kwa sasa limegeuzwa kama shamba la bibi.

No comments