Header Ads

Aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Mwanza Ajivua Uanachama


Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa.

Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la Chadema tangu Mei 4, mwaka jana, alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa.

Kwa uamuzi huo, Tizeba amepoteza nyadhifa zake zote ikiwamo ya uenyekiti wa Baraza la uongozi la mkoa na ujumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Ziwa.

Mei 5, mwaka jana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, wakati huo, Dk Willibrod Slaa, alimuandikia barua Tizeba yenye Kumb Na C/HO/ADM/KK/08 ,kumsimamisha uongozi wa chama hicho.

Akizungumzia uamuzi wa kiongozi huyo kujivua uanachama na kuachana na siasa, Mratibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Renatus Bujiku alisema chama hicho kimepokea kwa mshtuko taarifa hizo kwa sababu bado suala lake lilikuwa linashughulikiwa.

“Utaratibu wa chama ulikuwa unaendelea kushughulikia suala lake, nadhani kachukua uamuzi wa haraka,” alisema Bujiku.

No comments