Header Ads

MSN Is On Fire: Yazipita timu zaidi ya 90 Ulaya Kwa Ufungaji Msimu Huu Zikiwemo Bayern na Arsenal

Vijana watatu wa Ki-Amerika ya Kusini wa klabu ya BARCELONA Lionel Messi, Luis Suarez and Neymar wameendelea kuweka rekodi tofauti za ufungaji kila wanapocheza.
Mpya ya leo takwimu zinaonyesha washambuliaji hao watatu wamefunga magoli mengi msimu kuliko klabu ya Bayern Munich inayofundishwa na Pep Guardiola.
Vijana wa Pep Guardiola wapo kwenye mstari wa mbele wa kushinda ubingwa wa 4 mfululizo wa Bundesliga- lakini wamezidiwa kufunga magoli na wachezaji watatu tu wa Barca.
Ni Real Madrid, Paris Saint Germain, na FC Barcelona ndio timu pekee kutoka kwenye Top 5 ya ligi bora barani ulaya (EPL, Serie A, Bundesliga, Ligue 1, na La Liga) ambazo zimefunga magoli mengi kuliko ‘MSN’ katik msimu 2015-16.
Messi, Suarez na Neymar pekee yao wameshafunga magoli 97 – idadi ya magoli mengi kuliko zaidi ya vilabu 90.
Mshindi wa mara 5 wa tuzo ya Ballon d’Or jana alifunga magoli mawili dhidi ya Arsenal – hivyo kufanya idadi ya magoli waliyofunga Barca kuwa 129 na magoli 93 kati ya hayo yamefungwa na watoto wa Amerika ya kusini.  – idadi hii imezidiwa na Madrid ambao wamefunga magoli 95, na PSG wamefunga 94.
Bayern kwa upande wao wamefunga na magoli 86 – na magoli 56 yamefungwa na Robert Lewandoski na Thomas Muller.
Manchester City ndio wanaoongoza kwa kufunga magoli mengi katika mashindano yote – wamefunga magoli 74.
Wakati  Gunners wakiwa wanawaza namna ya kupambana mchezo wa pili – wanahitaji kuangalia namna walivyo nyuma walivyopitwa kwenye ufungaji – wamefunga magoli 61 tu kwenye mashindano yote.
CREDIT:SHAFII DAUDA

No comments