Header Ads

Mke wa Kafulila atimuliwa nje ya ukumbi wa bunge.


Mbunge wa Viti maalum Chadema Jesca Kishoa ametolewa nje ya ukumbi wa bunge na kutakiwa kutohudhuria vikao viwili vya bunge linaloendelea mjini Dodoma.

Hayo yamejiri katika mkutano wa 7 wa bunge la 11 linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambapo Mwenyekiti wa kikao cha leo Andrew Chenge amelikumbusha bunge kuhusiana na kauli aliyoitoa mbunge huyo tarehe 01/02/2016.
  
Mbunge huyo alisema kwamba Waziri Harrison Mwakyembe alihusika kununua mabehewa feki 274 jambo ambalo lilizua mjadala mkali na bunge kumtaka mbunge huyo atoe ushahidi ndani ya siku 3.

Mwenyekiti Andrew chenge amesema kuwa mbunge huyo alitakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge kanuni ya 63(6) atoe ushahidi kwa ofisi ya bunge na ndani ya siku zote ofisi ya bunge haijapata ushahidi huo.

Kutokana na Mbunge huyo ambaye pia ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila NCCR Mageuzi kushindwa kutekeleza maamuzi ya bunge mwenyekiti wa bunge amemtaka kufuta kauli yake na mbunge huyo akakaidi ndipo Mwenyekiti akamuamuru atoke nje mara moja na kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku zilizobakia 2.

No comments