RAIS MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI RAIS KIKWETE KWA KUFIWA NA DADA YAKE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.
Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia" Amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.
Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015
KIGOMA UJIJI YAPATA MEYA TOKA ACT WAZALENDO.
Madiwani wa Manispaa ya Kigoma ujiji wakiwa katika picha ya pamoja .
Mwenyekiti wa uchaguzi wa Meya na Naibu meya mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoa maelezo ya awali kabla ya uchaguzi.
Meya wa Manispaa ya kigoma Ujiji Hussein Ruhavi akimweleza jambo makamu meya Athuman Mussa wa manispaa hiyo kushoto ni mbunge wa Kigoma mjini ndiye alikuwa mwenyeti wa uchaguzi
Mmoja wa Madiwani akipiga kura ya kumchagua meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Kigoma Ujiji limemchagua Diwani wa kata ya Bangwe Hussein Ruhavi kuwa meya wa Manispaa hiyo.
Mbunge Zitto Zuberi Kabwe alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo alimtangaza diwani Ruhavi kutoka chama cha ACT wazalendo kuwa mshindi wa kiti cha umeya kwa kupata kura 19 kati ya kura 21 zilizopigwa na akamshinda mpinzani wake Masudi Kassim kutoka chama cha mapinduzi(CCM).
Pia Zitto alimtangaza diwani wa kata ya Buzebazeba Athumani Mussa kupitia chama cha ACT wazalendo kuwa naibu meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji alimshinda Mussa Maulid wa CCM aliyepata kura moja.
Baada ya kutangaza matokeo Zitto ambaye ni mbunge wa jimbo la kigoma mjini alisema kuwa watasimamia mipango ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa usawa.
"Diwani yeyote ambaye kwa makusudi ataamua kukwamisha michakato mbalimbalu ya maendeleo tutamshughulikia lwa namna tutakayojua sisi"alisema Zitto
Naye meya Hussein Ruhavi akizungumza baada ya kuchaguliwa aliwashukuru madiwani kwa imani yao waliyoionyesha kwake kwa kumchagua kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Alisema atafanya kazi kwa kushirikuana na madiwani wote ili kuwaletea wananchi maendeleo,pia aliwataka madiwani kufanya kazi pamoja bila ya kujali itikadi zao
SATURDAY, DECEMBER 19, 2015
SIMU TV: DONDOO ZA MAGAZETI LEO
SIMU.TV: Waziri awafungia geti wafanyakazi wa wizara. 12 wafariki ajali ya basi la New Force. CHADEMA yazungumzia kasi ya rais Magufuli;https://youtu.be/oZYeH59y4SI
SIMU.TV: Watumishi waliotumia vyeti feki serikalini kukiona cha moto. TMA yasema Elninyo kuendelea mpaka Aprili mwakani; https://youtu.be/wmJb-ZHmd4A
SIMU.TV: Kocha Kerr aficha mbinu. CCM Kirumba kuchimbika leo. Majabvi ashtukiwa, akatwa mshahara Simba, https://youtu.be/wqcG-CPluiU
SIMU.TV: Pata habari za kina zilizopewa kipaumbele katika magazeti ya leo Jumamosi Desemba 19.2015; https://youtu.be/yPokI-5bXwo
Post a Comment