Header Ads

UFISADI GEITA MIUNDOMBINU,AFYA BAADHI WAFIKISHWA MAHAKAMANI.

                         JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

                      TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA MKOA WA GEITA.
                                         Image result for TAKUKURU
Bw. Jossam Ntengeki-aliyekuwa mkandarasi wa stendi mpya ya mabasi ya Geita na mwenzake ambaye hakuwepo mahakamani wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Geita jana tarehe 02/07/2015 na kusomewa mashitaka manne ya rushwa yanayowakabili.
Akisoma mashitaka Bw.Celvin Murusuri mwanasheria wa TAKUKURU mbele ya Hakimu mkazi mheshimiwa Desidery Kamugisha alisema kuwa mtuhumiwa Bw. Jossam Ntengeki anatuhumiwa kutumia nyaraka mbalimbali kumdanganya mwajiri na kujipatia malipo hewa kwa kazi ambazo hazikufanyika.

Bw. Celvin Murusuri alisema kuwa kwa pamoja watuhumiwa hawa Bw.Ntengeki na mwenzake waliisababishia serikali hasara ya kiasi cha shilingi 17,342,110 kwa kutumia nyaraka za uongo kwa nia ya kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha PCCA na matumizi mabaya ya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha PCCA namba 11/2007.Watuhumiwa wote walikana mashtaka yote manne na kuachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Pia Bw.Frank Maganga aliyekuwa mhasibu wa idara ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Geita,alifikishwa mahakamani hiyo jana kwa kosa la kufanya manunuzi hewa ya vifaa vya hospitali na kuisababishia serikali hasara ya Tsh 12,450,000.

Akimsomea mashtaka mwendesha mashitaka wa serikali wa mkoa wa Geita Bw.Anosisye Erasto alisema kuwa Bw.Frank Maganga na mwenzake Bi.Angelina Mhando bohari wa Halmashauri ya wilaya ya Geita ambaye alisomewa mashitaka yake tarehe 19/06/2015 wanakabiliwa na makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11/2007,kughushi nyaraka kinyume na vifungu Na.333,335(a) na 337 vya kanuni ya adhabu sura ya ya 16/2002,kadhalika kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha kanuni ya adhabu.

Bw.Anosisye alimsomea mashitaka hayo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Geita,Mheshimiwa Desdery Kamugisha na kusema kwamba mwaka 2010/2011 watuhumiwa walifanya manunuzi hewa ya vifaa vya hospitali ya wilaya ya Geita  kutoka kwa Mwatulole General Supply and Printing vilivyokuwa na thamani ya Tsh.12,450,000.


Aidha washitakiwa walikana makosa yote matatu na waliachiwa baada ya kukidhi vigezo vya dhamana.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Bwana Thobias Ndaro anatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita watoe taarifa za vitendo vya Rushwa hata vile vinavyofanyika kwenye idara ya Afya ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.


IMETOLEWA NA MKUU WA TAKUKURU MKOA  WA GEITA .

No comments