AMAMA MBABAZI AZUIWA NA POLISI UGANDA.
Vyombo vya habari Uganda vinaarifu kwamba Kizza Besigye aliyekuwa mkuu wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) pia amekamatwa.
Inaarifiwa kwamba Polisi inamhamisha Amama Mbabazi kutoka Njeru eneo la kati mwa Uganda, na kumpeleka katika mji mkuu Kampala.
Haijulikani wazi ni kwanini anazuiwa na polisi.
Mbabazi amewahi kuonywa dhidi ya kufanya mikutanop ya umma kushinikiza azma yake ya kuwania urais.
Msaidizi wake binfasi Mbabazi amethibitisha kukamatwa kwake.
Tutakupasha taarifa zaidi pindi tutakapo zipokea.BBC
Post a Comment