Header Ads

MWINGINE TENA ATOKA NDUKI CCM.....!!!!





Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga, ametangaza kuihama CCM na  kuhamia  CHADEMA kutokana na kutokuwepo Demokrasia ya Kweli ndani ya CCM.

Dr. Mahanga ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake  kwenye Jimbo la Segerea  kwa  tiketi  ya  CCM  ametangaza azma hiyo jana mchana baada ya  rufaa yake ya kupinga ushindi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kipawa mama Kivela kutupiliwa mbali na Ofisi ya CCM mkoa wa Ilala.

Duru za Kisiasa zinasema kilichomponza Dr. Mahanga ni kitendo chake cha yeye kuhusika katika mpango wa kumnadi Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenye nafasi ya Urais wa CCM, ambaye kwa  sasa ametangaza kugombea urais kupitia Chadema.

No comments